Baada ya kumaliza majukumu ya ligi ya mabingwa na wakati wakisubiri kumfahamu mpinzani wao kwenye michuano ya kombe la Shirikosho, kikosi cha Yanga kinarejea katika ligi kuu ya Vodacom ambao keshokutwa Alhamisi kitakuwa dimba la Uhuru kuikaribisha Polisi Tanzania
Yanga iliyopoteza mchezo wake wa ufunguzi dhidi ya Ruvu Shooting, inahitaji ushindi kwenye mchezo huo
Polisi ilicheza na Yanga wakati wa maandalizi ya msimu na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0
Hata hivyo, kocha Mwinyi Zahera hakutumia kikosi chake cha kwanza kwenye mchezo huo
Mshambuliaji David Molinga ambaye hana leseni ya kushiriki michuano ya CAF, atarejea kikosini kuungana na kina Sadney Urikhob, Patrick Sibomana na Juma Balinya kuhakikisha Yanga inashinda
Jumapili Oktoba 06 Yanga itarejea tena dimba la Uhuru kuikabili Coastal Union
TUMEBORESHA APP YETU, TAFADHALI BOFYA HAPA CHINI KUDOWNLOAD APP YETU MPYA ILI KUENDELEA KUPOKEA HABARI KWA WAKATI NA KUTAZAMA MECHI ZOTE LIVE ( UKISHA BOFYA, BONYEZA NENO OPEN IN PLAY STORE KISHA INSTALL )BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YETU MPYA BURE KABISA
No comments:
Post a Comment