MFUNGWA mmoja amefariki na wengine saba kujeruhiwa baada ya gari la magereza kupinduka huko Kathageri karibu na Daraja la Thuci, Wilaya ya Embu, leo.
Pia askari watano wa magereza walipata majeraha na kupelekwa pamoja na wafungwa waliojeruhiwa, katika Hospitali ya Rufaa ya Chuka. Ofisa mfawidhi wa Gereza la Embu, Henry Ochieng, alisema lori hilo lilipinduka mara mbili wakati likiwa kwenye mteremko.
Aliongeza kwamba wafungwa hao walikuwa wakisafirishwa kutoka Gereza la Embu kwenda Mahakama za Meru ambapo pia dereva alijeruhiwa vibaya. na kupelekwa kwa matibabu katika Embu Level Five Teaching and Referral Hospital.
Shuhuda, Maureen Mwende, alisema ajali hiyo ilitokea asubuhi wakati wa mvua.
“Nafikiri ni kutokana na utelezi gari likashindikana kudhibitiwa,” alisema mwanamke huyo.
TUMEBORESHA APP YETU, TAFADHALI BOFYA HAPA CHINI KUDOWNLOAD APP YETU MPYA ILI KUENDELEA KUPOKEA HABARI KWA WAKATI NA KUTAZAMA MECHI ZOTE LIVE ( UKISHA BOFYA, BONYEZA NENO OPEN IN PLAY STORE KISHA INSTALL )
BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YETU MPYA BURE KABISA
No comments:
Post a Comment