We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Tuesday, October 1, 2019

"Faraja kuona mzigo wa korosho unaondoka" - Waziri Mkuu

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ametembelea bandari ya Mtwara na kushuhudia shehena ya korosho zilizonunuliwa na kampuni ya Tang Long zikipakiwa katika meli kubwa yenye jina la AS Christiana kwa ajili kusafirishwa kwenda nchini Vietnam.


Akizungumza katika eneo la bandari hiyo aliyotembelea leo Jumanne, Oktoba 1, 2019 kwa ajili ya kujionea kazi ya usafirishaji wa korosho inavyofanyika, Waziri Mkuu ameonesha kuridhishwa na kasi na utaratibu unaoendelea badarini hapo.
Ni faraja kuona mzigo wa korosho ukiondoka na kutoa nafasi ya kuingiza mzigo mwingine mpya wa korosho utakaopatikana baada ya kuanza msimu mpya mwezi huu. Na mnunuzi huyu ameahidi kununua tani 100,000 katika msimu wa mwaka huu”, amesema Waziri Mkuu Majaliwa.
Amesema kampuni ya Tang Long ya nchini Vietnam licha ya kuahidi kununua korosho katika msimu wa mwaka huu, pia imeomba kupatiwa eneo kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda cha kubangua korosho nchini na kwamba wapo tayari kuanza hata Desemba, 2019.
Waziri Mkuu pia amesema suala la ujenzi wa viwanda vya kubangulia korosho nchini litaongeza thamani na kuwezesha dunia nzima kutambua kuwa korosho hizo zimetoka Tanzania kwa sababu kwenye vifungashio watakuwa wameandika, hivyo kuongeza soko.
Akizungumzia kuhusu msimu wa uuzaji wa korosho wa mwaka huu, Waziri Mkuu amesema kipaumbele cha kwanza watapewa wenye viwanda vya ndani na kisha tani zinazobaki zitauzwa kwa wanunuzi kutoka nje.

TUMEBORESHA APP YETU, TAFADHALI BOFYA HAPA CHINI KUDOWNLOAD APP YETU MPYA ILI KUENDELEA KUPOKEA HABARI KWA WAKATI NA KUTAZAMA MECHI ZOTE LIVE ( UKISHA BOFYA, BONYEZA NENO OPEN IN PLAY STORE KISHA INSTALL )

BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YETU MPYA BURE KABISA

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list