We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Tuesday, September 3, 2019

Zitto na Lissu waipa nguvu ACT Wazalendo

Mshauri Mkuu wa Chama Cha ACT Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad, amesema kuwa, kuonekana pamoja kwa viongozi wawil vya vyama vya siasa vya upinzani, Zitto Kabwe (ACT) na Tundu Lissu (CHADEMA), kumewapa nguvu kuelekea uchaguzi wa 2020.

Maalim ameeleza kuwa wawili hao waliokutana nchini Ubelgiji ambako Tundu Lissu anaendelea na matibabu, wameonesha njia nzuri.
''Zitto Kabwe na Tundu Lissu wametupa faraja na kutuonesha njia kuelekea 2020. Nawapongeza na kuwatia moyo kutekeleza wajibu wa kihistoria kwa Tanzania wakati tunaelekea uchaguzi mkuu wa 2020 ambao ni uchaguzi muhimu kuliko chaguzi zote katika kuamua mustakabali wa Tanzania''.
Zitto Kabwe alirusha video mtandaoni ikionesha yupo na Tundu Lissu, wakitembea kwenye mitaa huko Ubelgiji huku wakisema mwanasheria huyo wa CHADEMA yupo tayari kurejea nchini.
Kwa mujibu wa ratiba aliyowahi kuitoa mwenyewe, Tundu Lissu atarejea nchini Septemba 7, ikiwa ni mara ya kwanza tangu alipoondoka kwenda kutibiwa mwaka 2017, kutokana na kujeruhiwa kwa kupigwa risasi mkoani Dodoma.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list