Kabla ya michezo ya kuhitimisha hatua ya awali michuano ya CAF, Msemaji wa Simba Haji Manara alikuwa mstari wa mbele kuwahamasisha mashabiki kuziunga mkono timu zote za Tanzania zinazoshiriki michuano hiyo yaani Azam Fc, KMC, Simba na Yanga
Lakini cha kushangaza kwenye mchezo kati ya Simba dhidi ya UD Songo, mashabiki wa Yanga walijitokeza kwa wingi uwanja wa Taifa kuiunga mkono Songo
Tukio hilo limemuibua tena Manara ambaye sasa amesema mashabiki wa Simba ruksa kuiunga mkono timu yoyote itakayokuja kucheza na Yanga, suala la uzalendo litabaki kwa Azam Fc tu!
"Wanasimba nawaomba radhi sana kuwaambia msiwashangilie wageni katika mechi zao ,wao wakawashangilia UD Songo"
"Sasa dini yangu inaruhusu kisasi hasa kwa watu wanaorejea kila siku makosa"
"Zesco nyie njooni bila mashabiki,huku mtatukuta tumejaa kuliko pishi ya mchele"
"Pa kufikia tushawaandalia!!, Yes uzalendo mwisho Azam fc"

No comments:
Post a Comment