Kikosi cha Yanga kiko jijini Ndola, Zambia tangu juzi jana wakijifua kwenye uwanja wa Mbinu unaomilikiwa na chama cha soka cha Zambia
Kuelekea mchezo wa kesho, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela, ambaye ndiye kiongozi wa msafara amesema timu iko kwenye mazingira salama na mipango ya kuhakikisha wanashinda kesho inakwenda vizuri
"Wachezaji wote wako katika hali nzuri, naamini tutatimiza malengo tuliyoweka kushinda mechi ya Jumamosi na kusonga mbele hatua ya makundi katika mashindano haya ya ligi ya mabingwa," amesema
Amesema kuwa morali ya kila mchezaji iko juu na kilichobakia ni kusubiri muda wa "mtangane" huo kuanza.
Leo Yanga itafanya mazoezi kwenye uwanja wa Levy Mwanawasa kwa mara ya kwanza
Mchezo wa kesho utapigwa kwenye uwanja huo ambao unachukua mashabiki 49,000
No comments:
Post a Comment