Muimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania, Rose Muhando ameachia wimbo wa kumsifu na kumshukuru Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta na wananchi wake kwa kumsaidia kipindi alipokuwa na matatizo ya afya.
Wimbo huo aliuachia siku ya Jumanne, Septemba 27, ambao unafanya vizuri kwa sasa katika mitandaoni.
"Shukrani zangu kwa taifa viongozi na wananchi wa Kenya kwa kuokoa maisha yangu, mlifungua milango yenu na kunikaribisha kwa mikono yenu miwili. Kwa hakika Kenya ilinionesha neema. Sijui jinsi ambavyo ninaweza kuwalipa kwa upendo wenu kwa kuwa mimi si tajiri lakini naomba Mungu aibariki Kenya", ni sehemu ya maneno yaliyopo katika wimbo huo wa Rose Muhando.
Ikumbukwe tu mwezi Novemba mwaka uliopita, zilisambaa video katika mitandao ya kijamii zikimuonyesha Rose Muhando akifanyiwa maombi ya kutolewa mapepo katika moja ya kanisa Jijini Nairobi kwa kudaiwa kutumia madawa ya kulevya.
Baada ya taarifa hizo shirikisho la muziki Tanzania “Tanzania Music Foundation” liliamuru Rose Muhando kurejeshwa nchini Tanzania kufanyiwa matibabu ambapo baada ya kurejea, kwa mara ya kwanza alionekana katika kanisa la Mlima wa Moto chini ya Mchungaji Bi. Gertrude Rwakatare.
No comments:
Post a Comment