Kikosi cha Yanga, mabingwa wa kihistoria Tanzania kiko nchini Zambia ambapo saa kumi jioni ya leo Jumamosi Septemba 28 kitakuwa uwanja wa Levy Mwanawasa kuikabili Zesco United katika mchezo wa marudiano ligi ya mabingwa
Timu hizo zinakutana kwa mara ya pili katika kipindi cha wiki mbili
Mchezo wa kwanza uliopigwa uwanja wa Taifa, ulimalizika kwa sare ya bao 1-1
Matokeo hayo yameufanya mchezo wa leo uwe wa kipekee kwa Yanga kwani inahitaji kushinda ili kujihakikishia nafasi ya kucheza hatua ya makundi ya michuano hiyo kwa mara ya pili katika historia yake
Licha ya kuwa Yanga inaweza kufuzu kwa matokeo ya sare ya kuanzia mabao mawili, lengo kuu ni ushindi
Yanga iliweka kambi ya takribani siku nne nchini Zambia kujiandaa na mchezo huo
Uongozi wa timu hiyo umetimiza wajibu wake kwa kuhakikisha timu inapata mazingira mazuri ya maandalizi, kazi iliyobaki ni kwa wachezaji kukamilisha ndoto ya Wanayanga kuiona timu yao inatinga makundi
Aidha kocha Mwinyi Zahera amesema wamejiandaa vyema, hawana wasiwasi kuelekea mchezo huo kwani wanafahamu kile wanachokwenda kukifanya kitawapa ushindi leo
Ni mchezo wenye presha kubwa kwa Yanga ambayo iko ugenini
Lakini Yanga imejijengea tabia ya kujiamini na kupata matokeo inapokuwa ugenini
Bila shaka utamaduni huo utaendelezwa na mashujaa hao ambao watakuwa wakipeperusha bendera ya Tanzania huko Zambia
No comments:
Post a Comment