Naibu waziri wa Nishati, Subira Mgalu ameeleza kusikitika kwa kitendo cha baadhi ya wananchi, ambao hawakujulikana kwa mara moja , kuchoma moto nguzo (60) za umeme, katika eneo la Kata ya Pande wilayani Kilwa, mkoani Lindi.
Naibu waziri Mgalu akizungumzia tukio hilo, amesema nguzo hizo zimechomwa maeneo ya Kata ya Pande, na kusema Serikali itahakikisha inawatia mbaroni wahusika wa tukio hilo, japo kwa sasa hawajajulikana.
"Nimesikitishwa sana nimepokea ujumbe hapa, kwamba kuna nguzo 60 za umeme zimechomwa moto huko Pande, hali hii haikubaliki hata kidogo." amesema Naibu Mgalu.
Mgalu amesema kutokana na uharibifu huo, zinahitajika zaidi ya Shil. Mil 30 kuirejesha hali hiyo, ambapo amedai ni kurudisha nyuma jitihada za Serikali katika kuwaondolea wananchi changamoto za umeme.
Aidha amewaomba viongozi wa Mkoa wa Lindi, washirikiane na vyombo vya ulinzi na usalama, kufanya upelelezi kwa lengo la kuwabaini wahusika na uchomaji moto wa gguzo hizo.
No comments:
Post a Comment