Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema Zesco United walipata bahati ya kuiondosha Yanga kwenye michuano ya ligi ya mabingwa
Akizungumza jana baada ya mchezo uliomalizika kwa Zesco kushinda mabao 2-1, Zahera alisema kikosi chake kilicheza vizuri na walitimiza malengo waliyokuwa wamejiwekea
"Tulipokuja hapa tulisema tunapaswa kufunga goli, huo ndio ulikuwa mpango wetu na tulifunga"
"Kilichotokea baadae ni bahati mbaya kwetu. Makame amelia sana kutokana na kujifunga, nimemwambia anyamaze"
"Ni matukio ya mpira. Wachezaji wakubwa huko Ulaya huwa wanajifunga pia, ni mpira"
Matokeo hayo yameipeleka Zesco hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa huku Yanga ikipata nafasi nyingine ya kuwania kutinga hatua ya makundi kombe la Shirikisho
Droo ya michezo ya mtoano inatarajiwa kufanyika wiki ijayo nchini Misri
No comments:
Post a Comment