Wachezaji wa Nkana Fc jana walikumbana na wakati mgumu kutoka kwa mashabiki wao baada ya timu hiyo kuchapwa bao 1-0 na Forest Rangers kwenye mchezo wa ligi kuu ya Zambia
Baada ya mchezo huo kumalizika, mashabiki waliwashambulia wachezaji kwa chupa, mawe huku wengine wakitumia manati kuwalenga kutoka jukwaani
Beki wa zamani wa Yanga, Mtanzania Hassani Kessy alikuwa miongoni mwa wachezaji hao ambao walilazimika kukimbia na kujificha maeneo mbalimbali ya uwanja kunusuru maisha yao
Nkana inashika nafasi ya nane kwenye msimamo wa ligi ya Zambia ikiwa imeshinda mechi mbili huku pia ikifungwa mechi mbili
Mashabiki walipata hasira baada ya timu hiyo kufungwa nyumbani
No comments:
Post a Comment