Zaidi ya kaya maskini 620,000 nchini China kupatiwa Runinga (32- nch LCD TVs) kwaajili ya kuhakikisha zinashuhudia sherehe za miaka 70 ya chama cha ‘Communist’ kinachotawala taifa hilo.
Wananchi hao wa Jamhuri ya watu wa China, kupatiwa seti nzima ya Runinga na Idara ya Umma ya chama hicho cha ‘Communist’ cha China (CPC) kupitia ofisi yake ya maadili, maendeleo, utamaduni, China Media Group na Radio ya taifa.
Hapo kesho Oktoba mosi taifa hilo lenyenguvu duniani linatarajia kuwa na Gwaride kubwa la kijeshi kwa ajili ya kusheherekea miaka hiyo 70 huku ikiahidi kuonyesha silaha zake mpya zinazotengenezwa nchini humo katika mji wa Beijing.
Gwaride hili limelenga kuwavutia wengi na litatumika kuonyesha vitu. Wizara ya ulinzi imeripoti kuwa wanajeshi 15,000 watashiriki pamoja na 59 ambao watatoka vikosi mbalimbali , huku silaha 580 zitaonyeshwa katika mitaa mbalimbali na ndege za kijeshi 160 zitarushwa angani.
Rais Xi Jinping atakagua gwaride hilo katika makutano ya Chang’an mjini Beijing na baada ya hapo ndege za jeshi zitaruka katika eneo la Tiananmen.
Kwa mara ya kwanza, askari 8,000 kutoka China ambao walikuwa mashujaa wa ulinzi wa amani wa Umoja wa mataifa wataweza kushiriki.
Jeshi la ‘People’s Liberation Army (PLA)’ lina shauku ya kuonyesha silaha mpya katika hadhara ambazo zimeshaanza kutumika.
No comments:
Post a Comment