Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo Septemba 2, 2019 amekutana na Watendaji wa Kata wa nchi nzima katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam. Kwa lengo la kuwapa miongozo ya kiutendaji ikiwemo kusimamia haki na kutatua kero za wananchi.
Rais Magufuli amesema kuwa “Sababu ya kuwaita hapa ni kuwapa meno ya kujitambua kuwa ninyi ni mabosi, sasa akatokee mwingine huko awaaambie ninyi sio mabosi, mwambieni aje aniambie mimi, nione kama ana ujasiri wa kusema hivyo.. “.
“Nitasikitika sana baada ya kikao cha leo atokee kiongozi yoyote niliyemteua mimi akamnyanyase kiongozi wa Kata, nitamwona hatoshi, lakini nitashangaa sana mtendaji wa Kata ambaye ananiwakilisha katika Kata ile aende akawaonee wananchi wangu maskini, waliokaa kwenye mvua na jua kunipigia kura,” Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
No comments:
Post a Comment