Baada ya Makamu Mwenyekiti Chama cha Wananchi CUF Taifa ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mtwara Mjini, Maftaha Nachuma kudai kuwa kamanda wa Polisi nchini IGP Simon Sirro anapendelea chama cha Mapinduzi (CCM), Katibu wa Jumuiya ya Vijana wa chama hicho Taifa (UVCCM) Raymond Mwangwala amemtaka mbunge huyo kuanza kufungasha virago vyake na kujiandaa kuachia jimbo hilo uchaguzi ujao.
Akizungumza wakati akizindua Mtwara ya kijani na kuelezea utekelezaji wa ilani ya CCM lakini pia maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa kwa mwaka huu amesema mbunge huyo na wapambe wake wanapaswa wajipange badala ya kukaa kwenye mitandao na kulialia.
Amesema chama hicho kimejipanga ili kuhakikisha kuwa majimbo yote yaliyochukuliwa na wapinzani yanarudi ndani ya chama hicho kuanzia uchaguzi wa serikali za mitaa.
“Nataka niwaambie jana wakati nikiwa njiani nakuja nimemuona mbunge wenu akilialia kwenye mitandao na bado hata yeye aanze kufungasha mizigo yake sasa ni zamu ya CCM apige kelele mvua inyeshe jua liwake giza liwe totoro lakini kuwe na mwanga jimbo hili nila CCM” amesema.
No comments:
Post a Comment