Mpango wa Neymar kurudi Barcelona umepiga mwamba baada ya mshambuliaji huyo wa Brazil mwenye umri wa miaka 27 ameamua kubaki kwa mabingwa wa ligue 1 Paris St- German.(Sun)
Matokeo yake kiungo wa Denmark mwenye miaka 27 ,Christian Eriksen aliyetaka kutoka Tottenham kwa paundi milioni 72 kwenda PSG imeshindikana.(Football.London)
Wakati huohuo uhamisho wa kiungo wa kati wa Tottenham na Denmark Christian Eriksen wa dau la Pauni milioni 72 kujiunga na PSG umeshindikana.(Express)
Lakini Eriksen bado ana nafasi ya kuondoka Spurs, Juventus wakijaribu kumyakua dakika za mwishoni.(Express)
Kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba, 27 anaweza kukataa kusaini mkataba mpya na Manchester United ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kusajiliwa Real Madrid. (Mirror)Ingawa meneja wa Unites Ole Gunnar Solskjaer amedai kuwa Pogba atasalia Old Trafford.(Express)
Bayern Munich inataka kumsaini winga wa Mancity Leroy Sane licha ya kwamba winga huyo mwenye umri wa miaka 23 atauguza jeraha la muda mrefu(Mirror)
Manchester United inawania kumuuza golikipa wake David de Gea mwenye umri wa miaka 29, na kusajili golikipa mpya mwezi januari . (Sun)
Rangers na Roma wanawania kumsajili kwa mkopo kiungo wa Manchester City Phil Foden, 19(Mirror)
Mamia ya mashabiki wa klabu ya Butty watahudhuria mechi itakayochezwa katika uwanja wa Gigg lane siku ya jumamosi baada ya kupigwa marufuku.
Mshambuliaji wa West Ham na Javier Hernandez, 31, ametuma maombi yake ya kuhamia Sevilla.(Mail)
Alexis Sanchez, 30,amejiunga na Inter Milan katika mkataba wa muda mrefu wa mkopo baada ya meneja wa Manchester United, Solskjae kumwambia kuwa mchezaji huyo anaweza kuchezea mashindano ya vikombe na ligi ya ulaya.(Sun)
Meneja wa Ranger Steven Gerrard amekata tamaa kumsajiri Ryan Kent, 22, kutoka klabu yake ya zamani ya Liverpool. (Express)
Mshambuliaji wa inter Milan Mauro icardi 26 ametishia kuishtaki klabu hiyo ya ligi ya serie A kwa kuwa mchezaji kiungo wa Argentina hana raha kuondolewa katika kikosi cha Kwanza cha timu hiyo.
Kiungo wa kati Ureno, Bruno Fernandes mwenye umri wa miaka 24 ,amekubali kuhamia Tottenham kutoka klabu ya sporting lisbon lakini klabu hiyo ya ligi ya uhispania imezuia uhamisho huo.
Mshambuliaji wa Juventus na Argentina Paulo Dybala, 25, hataondoka klabu hiyo kabla ya dirisha la jumatatu halijafungwa, mwenyekiti wa klabu alisema.(Goal)
Golikipa wa Hispania Sergio Rico, 25, yuko mbioni kutoka Sevilla kuhamia Paris St-Germain .(Le Parisien)
Klabu ya ujerumani ya Borrusia Dortmund ndio klabu ya hivi karibuni kuonyesha hamu ya kumsajili mshambuliaji wa Liverpool Bobby Dancun 18 huku klabu hiyo ya bundesliga ikifikiria kuwasajili wachezaji zaidi wa Uingereza pamoja Jadon sancho
No comments:
Post a Comment