Taarifa iliyotolewa leo Jumatatu Septemba 2, 2019 na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu ya Tanzania, imemnukuu Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi akisema uteuzi wa Profesa Kahimba umeanza Agosti 31, 2019.
Balozi Kijazi amesema kabla ya uteuzi huo, Profesa Kahimba alikuwa Profesa Mshiriki na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo (Utawala na Fedha), Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) mkoani Morogoro.
Taarifa hiyo imesema Profesa Kahimba amechukua nafasi hiyo iliyokuwa wazi.
No comments:
Post a Comment