Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam leo Jumatatu, Septemba 2, 2019, imeendelea na usikilizaji wa maombi ya aliyekuwa mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, ya kibali cha kufungua shauri kupinga kukoma kwa ubunge wake.
Kiongozi wa jopo la mawakili wa Lissu, Peter Kibatala, amewasilisha hoja za kuomba kibali katika hoja zake pamoja na mambo mengine amesema kuwa hatua zilizochukuliwa na Spika Job Ndugai kutangaza kuwa kiti cha Lissu kiko wazi kilifanyika bila haki ya upande wao kusikilizwa.
Kiongozi wa jopo la mawakili wa Lissu, Peter Kibatala, amewasilisha hoja za kuomba kibali katika hoja zake pamoja na mambo mengine amesema kuwa hatua zilizochukuliwa na Spika Job Ndugai kutangaza kuwa kiti cha Lissu kiko wazi kilifanyika bila haki ya upande wao kusikilizwa.
Kibatala ameeleza hakupewa haki ya kusikilizwa kabla ya uamuzi huo na kwamba wala hakuwahi kuelezwa sababu za kukoma kwa ubunge wake, huku akidai Spika ambaye ndio alikuwa mlalamikaji na jaji katika kesi yake hiyo.
Wakili Kibatala ambaye katika hoja zake amewasilisha mahakamani kesi mbalimbali zilizokwishakuamuriwa na Mahakama Kuu, Mahakama ya Rufani na hata mahakama za nje, amesema jambo ambalo ni kinyume cha misingi ya haki ya asili ya kusikilizwa kabla ya kuhukumiwa.
Amesema kwa mujibu wa maombi katika viapo vyao kinzani, wanatoa tafsiri ya kifungu cha 37(3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi kumtaarifu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa kiti cha jimbo la Singida Mashariki kiko wazi si tamko la kumvua ubunge.
Hata hivyo, amesema jukumu la kutafsiri sheria ni la Mahakama na si la mtu mwingine yeyote.
Advertisement
Katika hatua nyingine, Wakili Kibatala ameiomba Mahakama hiyo itoe amri za kusitisha kwa muda kuapishwa kwa mbunge mteule wa jimbo hilo Miraji Mtaturu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), kusubiri kumalizika kwa mashauri hayo.
Wakili Kibatala ameieleza mahakama kuwa vikao vya Bunge vinatarajia kuanza kesho Jumanne na kwamba kwa mujibu wa taratibu za bunge moja ya shughuli zitakazofanyika kabla ya shughuli nyingine za kawaida za Bunge ni kuapishwa kwa Mtaturu.
“Kama Mtaturu akiapishwa, Mheshimiwa Jaji kazi ya Mahakama hii itakuwa ngumu na hata kwa mwombaji itakuwa vigumu kulinda haki zake. Na hata mwenendo huu hautakuwa na maana,” amesema wakili Kibatala
“Kwa misingi hii Mahakama inaweza kutoa amri kuhusu ombi si (kusimamisha kwa muda kuapishwa kwa Mtaturu), hata kabla ya kutoa uamuzi wa ombi la kibali.”
Pamoja na mambo mengine pia Kibatala ameelezea mazingira ya Lissu kushindwa kuhudhuria vikao vya Bunge pamoja na kutoa tamko la mali na madeni yake katika Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma akisema ni kwa sababu ya ugonjwa.
Katika hilo, Wakili Kibatala pia ameelezea tukio zima la kushambuliwa kwa Lissu akirejea maelezo ya Lissu mwenyewe katika maelezo yake ya maandishi pamoja na hati za viapo vinavyounga mkono maombi hayo.
No comments:
Post a Comment