Ukizungumzia wachezaji waliofanya vizuri kwenye kikosi cha Yanga jana katika mchezo dhidi ya ZESCO United, kiungo Abdulaziz Makame 'Bui' ni mongoni mwao
Yanga ilikuwa bora sana kwenye kipindi cha kwanza cha mchezo huo uliomalizika kwa sare ya bao 1-1
Wachezaji walitengeneza nafasi lakini changamoto ya kutumbukiza mipira kimiani iliendelea kuitesa Yanga
Akizungumza baada ya mchezo Makame alisema waliruhusu bao kwenye dakika za majeruhi baada ya kupoteza umakini
Aidha Makame amesema wanahitaji kufanyia kazi safu yao ya ushambuliaji ili waweze kutumia nafasi wanazotengeneza
"Ni makosa tulifanya, tulipoteza umakini wenzetu wakatumia nafasi hiyo kusawazisha," Bui aliiambia Azam Tv
"Tunajipanga kuelekea mchezo wa marudiano lakini nadhani tunapaswa kufanyia kazi mbele (ushambuliaji) kwani tumetengeneza nafasi nyingi tukashindwa kuzitumia"
Yanga ina kazi ya kwenda kupindua matokeo nchini Zambia Septemba 26 kama ilivyofanya mchezo dhidi ya Township Rollers
Kocha Mwinyi Zahera amesema watajipanga kuhakikisha wanapata matokeo nchini humo

No comments:
Post a Comment