Kiungo wa Manchester United na Uskochi Scott McTominay, 22, ametaka watu wamvumilie kocha Ole Gunnar Solskjaer. (Mirror)
Solskjaer amethibitisha kuwa Manchester United itaingia sokoni kutafuta mshambuliaji na kiungo mchezeshaji ili kuboresha nguvu ya mashambulizi ya klabu hiyo ambayo imeshindwa kufunga zaidi ya goli moja kwenye michezo 17 kati ya 20 iliyopita. (Telegraph)
Arsenal wanataka kumtoa kwa mkopo kiungo Mjerumani Mesut Ozil, 30, mwezi Januari, hata kama itawalazimu kutoa ruzuku ya mshara wake kwa timu atakayoenda. (Mirror)
Kocha wa Inter Milan Antonio Conte anawekeza nguvu zake katika kumsajili kiungo wa kimataifa wa Serbia kutoka klabu ya i Manchester United Nemanja Matic, 31. (Calciomercato)
Manchester United wanatarajiwa kujaribu tena kumsajili msahambuliaji wa timu ya taifa ya Croatia na klabu ya Juventus Mario Mandzukic, 33, ambaye alikuwa kwenye mipango yao kwenye dirisha la usajili lililopita. Juve wanatarajiwa kutaka ada ya uhamisho ya pauni milioni 9, huku Mandzukic akitarajiwa kukataa ofa yoyote ya mshahara chini ya kiwango anacholipwa sasa cha pauni milioni 4.5 kwa mawaka. (Goal.com)
Mandzukic amevunja mazungumzo na klabu ya Al Rayyan na sasa hatajiunga na timu hiyo kutokea nchini Qatar. (Goal.com)
Klabu ya PSV Eindhoven ya Uholanzi inataka kumsajili kwa mkopo kiungo wa Manchester United na timu ya taifa ya Uholanzi ya chini ya miaka 21Tahith Chong. (Sun)
Mshambuliaji wa klabu ya Napoli na timu ya taifa ya Ubelgiji Dries Mertens, 32, anajianda kuondoka kwenye klabu hiyo kama mchezaji huru mwishoni mwa msimu. (Calciomercato)
Kocha wa Arsenal Unai Emery amekanusha kuwa ana matatizo ya lugha na hivyo kushindwa kuelewanan na wachezaji wake - japo anasema Kingereza chake ni kizuri kwa alama sita kati ya 10. (Mirror)
Kiungo wa zamani wa Arsenal Emmanuel Petit amemuonya Emery dhidi ya kubadili kikosi mara kwa mara. (Sun)
Kocha wa Stoke ambaye yupo kwenye wakati mgumu Nathan Jones amesisitiza kuwa bado anaimani na uwezo wake na anaamini yeye ndio mtu sahihi wa kuinoa kalabu hiyo. (Stoke Sentinel)
Kocha wa klabu ya Celtic ya Uskochi Neil Lennon amesisitiza kuwa mkuu wa usajili wa klabu hiyo Nick Hammond yupo kibaruani kumpatia machaguo ya kukiboresha kikosi chake kuelekea dirisha la usajili la mwezi Januari. (Star)
No comments:
Post a Comment