We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Saturday, September 28, 2019

Tetesi za usajili barani ulaya Leo Jumamosi

Paul Pogba ameiomba Man United kumpatia kandarasi mpya yenye thamni ya £600,000 kwa wiki . Kiungo huyo wa kati wa Ufaransa ,26, anajua kwamba ananyatiwa na Juventus pamoja na Real Madrid. (Tuttosport - in Italian)
Wachezaji wa Spurs wamekasirishwa na mkufunzi Mauricio Pochettino baada ya kusema kwamba walikuwa na ajenda tofauti wakati waliposhindwa na Colchester katika kombe la Carabao siku ya Jumanne.. (sun)
Manchester United inafikiria kumsajili kiungo wa kati wa Tottenham Christian Eriksen, 27, huku Spurs ikijiandaa kutokosa huduma za kiungo huyo wa Denmark katika uhamisho wa bure mwisho wa msimu huu. (Goal)

Manchester United inafikiria kumsajili kiungo wa kati wa Tottenham Christian Eriksen, 27

Mshambuliaji wa Paris St-Germain Neymar na klabu yake ya zamani Barcelona bado hawajatatua mzozo kuhusu malipo ya uaminifu baada ya makubaliano ya kuzuia kuipeleka kesi hiyo mbele ya jopo la mahakama kugonga mwamba.. (Sky Sports)
Mawakili wanaomwakilisha Neymar na Barcelona wameafikia siku nyengine ya pili mnamo tarehe 21 Oktoba.. (ESPN)
Mchezaji wa Brazil Neymar, 27, alikuwa tayari kufutilia mbali kesi hiyo iwapo Barcelona ingejitolea kwa maandishi kumsaini tena. (Cadena SER - in Spanish)

Neymar JR

Mkufunzi wa Jose Mourinho anataka kurudi Real Madrid, baada ya kukataa ofa kutoka Monaco, Lille, Wolfsburg, Schalke na AC Milantangu alipofutwa kazi na klabu ya Manchester United mwaka uliopita . (Goal)
Mkufunzi wa Man United Ole Gunnar Solskjaer amemchagua skauti wake wa kibinafsi kutazama wachezaji anaowalenga katika dirisha la uhamisho. (Sun)
Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp amesema kwamba hana wasiwasi kuhusu hali ya kiungo wa kati wa timu hiyo James Milner, 33, kuwa katika mwaka wa mwisho wa kandarasi yake . (Guardian)
Mkataba wa sare mpya ya Liverpool inayodhaminiwa na kampuni ya sare za michezo una thamani wa £15m kwa mwaka chini ya mktaba wao sasa na kmapuni ya New Balance, ambayo inatoa £45m kwa mwaka. (Times)
Mshambuliaji wa Juventus na Argentina Gonzalo Higuain, 31, ametoa ishara ya kutaka kurudi katika klabu yake ya zamani ya River Plate kandarasi yake itakapokamilika 2021. (Fox Sports Radio Argentina - in Spanish)
Rais wa Bayern Munich Uli Hoeness anasema kwamba huenda klabu yake ikaimarisha upya hamu yake ya kutaka kumsajili winga wa ujerumani na Manchester City Leroy Sane, 23, mwezi Januari. (Planet Futbol via Sky Sports)
Kiungo wa kati wa Newcastle Sean Longstaff, 21, anasema kwamba alivutiwa na hamu kutoka man United msimu huu lakini anasisitiza kuwa makubaliano yoyote yatategemea klabu zote mbili.. (Times - subscription required)
Southampton na Manchester City zinamnyatia beki wa klabu ya Hearts mwenye umri wa miaka 17Aaron Hickey. (Daily Record)
Aliyekuwa afisa mkuu mtendaji wa Manchester United na Chelsea Peter Kenyon anajaribu kumshawishi mmiliki wa klabu ya Newcastle Mike Ashley kuhusu mpango wa malipo wa kuinunua klabu hiyo kwa niaba ya wawekezaji wa Marekani. (Sun)
Peter Kenyon pia alifanya mazungumzo na kampuni hiyo ya uwekezaji MSD Partners, ambao wanainunua klabu pinzani ya Newcastle iliopo kaskazini mashariki Sunderland. (Mail)
Mkufunzi Steve Bruce anasema kwamba hajali kuhusu mazungumzo ya ununuzi wa klabu hiyo akitaja kuwa swala ambalo limekuwa likiendelea.". (Mirror)
Aston Villa imepewa £7m kumuuza mchezaji wa Ivory Coast onathan Kodjia, 29, na klabu ya Qatari Al-Gharafa. (Football Insider)
Mshambuliaji wa Nice Lamine Diaby-Fadiga amekiri kumuibia mchezaji mwenza Kasper Dolberg saa yenye thamani ya ' Yuro 70,000 . (ESPN)

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list