Mwekezaji wa klabu ya Simba Bilionea Mohammed Dewji 'Mo' leo alitembelea viwanja vya klabu hiyo ambavyo viko kwenye matengenezo Bunju nje kidogo ya jiji la Dar es salaam
Mo ameeleza kuridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa viwanja hivyo ambapo amesema hadi kufikia mwishoni mwa mwezi ujao (Oktoba), Simba itaanza kufanya mazoezi
"Leo asubuhi nilitembelea viwanja viwili vya mazoezi vya Simba vilivyopo Bunju kuangalia maendeleo," ameandika Mokwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instargam
"Nina habari njema, kufikia mwishoni mwa mwezi Oktoba, uwanja wa nyasi asilia na nyasi bandia pamoja na vyumba vya kubadilishia nguo vitakuwa vimekamilika"
"Insha'Allah! Natarajia kuona timu ikifanya mazoezi hivi karibuni"
No comments:
Post a Comment