Mchekeshaji maarufu Pierre Liquid amesema kuwa kwa siku anao uwezo wa kunywa bia 38 kwa kuwa ndiyo kinywaji pekee anachokipenda na huwa kinachompa raha.
Hayo ameyabainisha wakati akizungumza na EATV & EA Radio Digital wakati wa sherehe ya kumbukizi ya kuzaliwa kwa mrembo Wema Sepetu, iliyofanyika usiku wa kuamkia Septemba 28 Jijini Dar es Salaam.
''Mimi kama mimi sina ugomvi na mtu, mimi napenda kunywa gambe, nafurahi kama hivi na kwa leo nimekunywa bia 38 na nikimaliza chupa naziweka chini'', amesema Liquid.
Akizungumzia ishu ya kumpenda Wema, Pierre amedai kuwa yeye na Wema wanapendana kwa dhati lakini anavutiwa zaidi na Jackline Wolper na hata kama angeambiwa achague mwanamke kati ya Gigy Money, Vanessa Mdee, Aunty Ezekiel lakini bado angemchagua Wolper.
"Wema ni mshkaji wangu, mpenzi wangu nampenda na yeye ananipenda, katika maisha tunatakiwa tupendane na Mungu anapenda tupendane, Mimi namuombea aishi miaka mingi zaidi hata ifike 120, Wema wangu Mungu amlinde na amtie nguvu", amemalizia Pierre.
No comments:
Post a Comment