Uongozi wa klabu ya Simba mwanzoni mwa msimu uliweka wazi kuwa hautavumilia utovu wa nidhamu ambao utafanywa na wachezaji wake
Kiungo Jonas Mkude hakusafiri na timu kanda ya ziwa huku ikielezwa kuwa aliondoka kambini bila kutoa taarifa kwa mtu yeyote akiwemo Meneja wa Simba Patrick Rweyemamu
Tukio hilo linaelezwa kumkera Patrick Aussems, kocha wa mabingwa na vinara hao wa ligi kuu
Inaelezwa Mkude ametakiwa kujieleza kwa maandishi sababu zilizopelekea kuondoka kambini
Miongoni mwa adhabu anazoweza kukumbana nazo kama uongozi hautaridhika na sababu zake, ni pamoja na kukatwa mshahara au hata kusimamishwa kwa michezo kadhaa
No comments:
Post a Comment