Mshambuliaji wa zamani wa Simba Laudirt Mavugo amesajiliwa na Difaa El Jadida ya Morocco
Kulingana na taarifa iliyotolewa na timu hiyo, Mavugo amesaini mkataba wa miaka miwili. Katika klabu hiyo, ameungana na Watanzania Saimon Msuva na Nickson Kibabage
Msimu uliopita Mavugo aliitumikia Napsa Stars ya Zambia, akiibuka miongoni mwa wafungaji bora wa ligi hiyo
Mavugo aliondoka Simba misimu miwili iliyopita baada ya kutokuwa na mwenendo mzuri katika klabu hiyo
Ni mchezaji mwenye kipaji, lakini pengine alikosa bahati kun'gara kwenye soka la Tanzania
No comments:
Post a Comment