Lugola alitoa agizo hilo jana jioni Jumapili Septemba 29, 2019 kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika stendi ya Majimoto Halmashauri ya Mlele mkoani humo wakati akijibu kero za wananchi.
Alisema kupitia kero zilizowasilishwa na wananchi, zinaonyesha wazi askari hao 15 wanajihusisha na rushwa, kupiga wananchi ovyo wakiwemo bodaboda, kushindwa kudhibiti ulinzi na usalama na kutoshughulikia malalamiko ya wananchi.
"Nataka niseme haya kutoa mfano, ili iwe fundisho kwa wengine kote nchini, Kaimu kamanda, natoa siku saba askari wote wa kituo hiki wahamishwe na waletwe wengine ili wajifunze," alisema Lugola.
Baada ya agizo hilo, Waziri Lugola aliwauliza wananchi askari wote wanatakiwa kuhamishwa? ambapo walipinga mkuu wa kituo hicho Iddy Kombo asihamishwe badala yake wahamishwe askari wengine wote.
"Asihamishwe, asihamishwe, asihamishwe," walisema wananchi.
Hata hivyo, Waziri Lugola alitii maoni ya wananchi na kuamuru mkuu huyo wa kituo pekee asihamishwe kituo cha kazi.
No comments:
Post a Comment