Abiria waliokuwa wakisafiri na Basi la Kampuni ya Arizona kutoka mkoani Kigoma kuelekea jijini Dar es salaam, wamegoma kuendelea na safari baada ya kufika Tabora na kubaini uwepo wa Kunguni katika viti vya basi hilo.
Baadhi ya abiria wameleeza malalamiko yao juu ya usafiri huo kwa kudai kuwa hawawezi kuendelea na safari hiyo kwa sababu kunguni wamezidi.
Akizungumzia hali hiyo, Hamisi Mshihiri ambaye ni Kamanda wa kitengo cha ukaguzi wa Mabasi Mkoa wa Tabora, amesema baada ya gari kufika mkoani humo alichukuwa jukumu la kuzuia basi hilo kutokana na kukosa vigezo pamoja na kuwa na mapungufu ya usafi.
"Mimi kama Mtaalam wa Magari na mwenye dhamana eneo hili, baada la kulijaribu nimeona gari hili lina mapungufu ya ufundi na usafi, kwa kweli hatuna namna nyingine zaidi ya kulizuia, kwa sababu abiria wanateseka” amesema Kamanda Hamisi Mshihiri
Serikali ipo katika mpango wa kuweka vituo maalum vya ukaguzi wa Mabasi katia kila vituo vikuu vya Mabasi kwa kila Mkoa, ambapo mabasi ya abiria yatafanyiwa ukaguzi kabla ya kuanza safari na mwisho wa safari.
No comments:
Post a Comment