We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Sunday, September 29, 2019

Hatutoi fidia kwenye mradi wa REA - Waziri Kalemani


Na Rahel Nyabali, Tabora

Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani amesema   serikari haitolipa  fidia kwa  wananchi  wenye  maeneo  yanayopitiwa  na  mradi  wa  umeme  vijijini  REA kwa  kuwa  mradi  huo  ni  wa  maendeleo yanayoihusu  jamii  yenyewe  hivyo  wananchi  wanatakiwa  kuchangamkia  fursa  hiyo ya umeme  vijijini katika  kubadilisha  hali  zao  kiuchumi.

Ameyasema hayo akiwa katika katika kijiji cha Mwambaha wilayani nzega mkoani Tabora na kutoa   msimamo  huo  wa  Serikali  wakati  akizungumza  na  wananchi  alipokuwa  akikagua  kazi  ya  utekelezaji  ujenzi  wa  miundombinu  ya  umeme  wa  REA awamu  ya  tatu  wilayani  humohuku  akitoa  wito  kwa  wananchi  kushirikiana  na Serikali  katika  utunzaji  ya  miundombinu  ya  umeme  huo  wa  REA.

Hatahivyo Dr.Kaleman  amemsisitiza  mkandarasi  kampuni  ya Pomy  Electrical  LTD anayetekeleza mradi huo kuhakikisha anakamilisha kazi  aliyopewa ya  kusambaza umeme  katika  vijiji  vipatavyo  36 vya wilaya ya nzega  ifikapo mwezi dec mwaka huu  ambapo  mkandarasi  alionesha  kufanyakazi  kwa  kusuasua  ingawa  kwasasa  jumla  ya  vijiji  ishirini  vimekwishawashiwa  umeme.

“Mkandalasi unatakiwa ifikapo mwezi wa kumi nambili mwaka huu uwe umekamilisha kusambaza Umeme katika maeneo yote hii itasaidia wananchi kuongeza uchumi katika familia na taifa kwa ujumla” amesema Kalemani

Edda Kaijage,Afisa mtendaji kijiji cha Mwambaha amesema Upatikanaji wa umeme ambao  utawasa wanakijiji  kwa kuutimia katika   fursa  mbalimbali na kusaidia  kufikia uchumi wa kati kupitia viwanda.

“Kupatikana kwa Umeme vijijini kutasaidia kwa kiasi kikubwa wananchi kujiinua kiuchumi kwa kuanzisha viwanda vidogovidogo jambo ambalo litasaidia kuwaongezea kipato wananchi na taifa kwa ujumla” Amesema Edda

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list