We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Sunday, September 15, 2019

Kenya : Watanzania mbaroni wakijifanya walemavu

Jeshi la Polisi Kenya linawashikilia Watanzania 6 kwa tuhuma za kufanya shughuli za ombaomba eneo la Makueni, lilipo Mashariki mwa nchi hiyo.


Kamanda wa Polisi wa Makueni Joseph Ole Napeiyan, amesema Watanzania hao wamekuwa wakitumia viti vya watu wenye ulemavu, na kufanya shughuli zao za kuomba katikati ya Makueni.
Siku za hivi karibuni tulipokea malalamiko kutoka kwa  wakazi wa maeneo ya Migori wakilalamikia kuwepo kwa watanzania hao ambao wamekuwa wakifanya shughuli hizo za kuomba msaada kwa wakenya” Amesema RPC Makueni, Joseph Ole Napeiyan
Ameongeza kuwa kati ya hao Watanzania 6, mwanaume ni 1 na wanawake 5 huku mwanamke mmoja akiwa na mtoto, na kueleza jeshi hilo kuwashikilia kwa ajili ya uchunguzi.
Hivi karibuni uongozi wa Serikali eneo la Migori, uliomba Serikali ya Kenya kuwaondoa ombaomba wote wa Kitanzania waliopo nchini humo.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list