We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Tuesday, September 17, 2019

Kauli ya Mtaturu baada ya Rais kumsifia hadharani

Mbunge  wa Jimbo la Singida Mashariki Miraji Mtaturu, ameonesha ni kwa namna gani ambavyo hakutegemea kama Rais Magufuli, angefurahishwa na uwepo wake kama mwakilishi wa wananchi katika jimbo hilo.


Mtaturu ameyabainisha hayo leo Septemba 17, 2019, ikiwa ni siku moja imepita tangu Rais Magufuli alipompongeza na kuiagiza Wizara ya Maji, kuhakikisha inatatua changamoto na kero ya maji  kupitia hoja aliyoiwasilisha Bungeni wakati akila kiapo siku ya Septemba 3, 2019.
''Kwahiyo nimefurahi namna ambavyo Mheshimiwa Rais amelipokea na kuelekeza Wizara ilifanyie kazi, kwahiyo mimi ntafuatilia ili kuhakikisha hiyo ahadi inatekelezwa na huduma inatolewa kwa wananchi'' amesema Mtaturu.
Aidha Mbunge Mtaturu ameongeza kuwa, licha ya uwepo wa changamoto hiyo kuzaa matunda kwa kuahidiwa itatuliwa kwa uharaka, amesema kuwa  Septemba 20 anatarajia kurudi jimboni kwake na kukutana na wananchi na kuchapa kazi kama alivyowaahidi.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list