Yanga huenda ikaongeza nguvu safu ya ulinzi upande wa kushoto wakati wa usajili wa dirisha dogo ambapo beki Erick Rutanga anatajwa kuelekea Jangwani
Wakati wa usajili uliopita, Yanga ilimuwania Rutanga lakini walishindwa kufikia makubaliano na timu yake Rayon Sports
Kwenye nafasi hiyo, kwa sasa Yanga inawategemea Muharami Issa 'Marcelo' na Ally Mtoni ambaye kwa asili ni beki wa kati
Mtoni ameaminiwa zaidi na kocha Mwinyi Zahera katika michezo ya hivi karibuni
Rutanga ni aina ya beki wa pembeni mwenye uwezo mkubwa katika ulinzi na mahiri kwenye kupeleka mashambulizi mbele

No comments:
Post a Comment