We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Tuesday, September 17, 2019

RC Makonda: Sijalala ile kauli ya Rais Magufuli / Nigejiuzulu kama ningekuwa sina njaa

Makonda aunda tume kushughulikia miradi ya kimkakati Dar Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ameunda tume itakayoongozwa na katibu tawala wa mkoa huo Abobakar Kunenge kushughulikia miradi ya kimkakati inayotekelezwa na serikali kuu katika Mkoa wa Dar es salaam. Makonda ametoa taarifa ya kuundwa kwa tume hiyo wakati akizungumza na watendaji na wazazi wa wanafunzi waliopatiwa ufadhili wa kusoma kwa wanafunzi wa kike wa kidato cha tano waliofaulu masomo ya Sayansi kupitia mfuko aliouanzisha. Mkuu wa Mkoa ameunda tume hiyo kufuatia maelekezo yaliyotolewa na Rais Dkt John Magufuli ya kuwataka viongozi wa mkoa wa Dar es salaam kusimamia kwa ukaribu miradi inayotekelezwa na serikali katika mkoa huo. Katika maelekezo hayo Mhe Rais kwanza alionesha kukerwa na ucheleweshwaji wa miradi ya Machinjio ya Kisasa eneo la vingunguti na mradi wa uboreshaji wa eneo la Coco Beach. Baada ya maelekezo hayo Mkuu huyo wa Mkoa ametangaza kuunda tume itakayosimamia miradi mnne inayotekelezwa na serikali kuu katika mkoa wa Dar es salaam ambayo ni ujenzi wa soko la Kisutu, Ujenzi wa Machinjio ya kisasa Vingunguti, Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha mabasi yaendayo mikoani cha Mbezi na Ujenzi wa Ufukwe wa Coco.

Bonyeza play hapa chini kutazama zaidi pia tembelea app hii kila Mara kusoma habari mpya


No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list