Naibu Waziri wa kilimo Hussein Basheamesema kwa mujibu wa ripoti ya ukaguzi ya shirika la Ukaguzi wa Vyama vya Ushirika (COASCO), wamebaini kuwepo kwa upotevu wa jumla ya shilingi Bilioni 123 kwenye vyama vya ushirika.
“Hapa nina kabrasha, nitawapatia wakuu wa mikoa wote, na nitamkabidhi kiongozi wa tume, kwa ripoti ya COASCO ushirika kumetokea jumla ya upotevu wa sh. Bilioni 123, na nisema hapa hatua kali zitachukuliwa kwa wahusika wote,” Bashe
“Hizi ni pesa za wakulima, wote waliohusika katika huu upotevu watachukuliwa hatua kali, na wakuu wa mikoa tutawapa majina ya Amcos gani wanahusika na mnatakiwa kuchukua hatua,” Bashe.
No comments:
Post a Comment