ASKARI wawili wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) kikosi cha 24KJ Mkoani Kigoma, wamefariki dunia na wengine 20 kujeruhiwa katika ajali iliyotokea leo, Septemba 26, 2019 kwenye hifadhi ya Katavi.
Askari hao wamepata ajali baada ya gari la jeshi lililokuwa limebeba silaha kupinduka wakati wakielekea kwenye oparesheni Mkoani Katavi.
Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma, Maweni Lameck Mdengo amethibitisha kupokea majeruhi hao pamoja na maiti mbili.
“Ili kuwa majira ya saa 8 tulipokea majeruhi 20 na wawili wakiwa wamefariki dunia ambao tumewapatia huduma ya kwanza, wapo waovunjika mikono na miguu pia lakini tunafanya utaratibu kuwapa rufaa ya kwenda Muhimbili au Bugando,” alisema na kuwataja waliofariki ni Bakari Juma Mohamed, Rashid Abed Mwimbe.

No comments:
Post a Comment