Pamoja na timu yake kulazimishwa sare ya bao 1-1 na ZESCO United leo kwenye mchezo wa duru ya kwanza michuano ya ligi ya mabingwa, kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema bado wana nafasi ya kufanya vizuri kwenye mchezo wa marudiano nchini Zambia
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mchezo huo, Zahera amewapongeza wachezaji wake kwa mchezo mzuri
"Kwa ujumla timu imecheza vizuri, wachezaji walijaribu kutumia nafasi tulizotengeneza"
"Matokeo haya hayatukatishi tamaa kwani bado nafasi ya kufanya vizuri ugenini tunayo"
"Tunapaswa kufunga bao nchini Zambia, hata kama tungeshinda bao 1-0, bado tungepaswa kufunga bao ugenini"
"Tutakwenda kuwafunga huko huko kwao," amesema Zahera
Matokeo ya leo hayana tofauti na matokeo ya mchezo wa hatua ya awali kati ya Yanga dhidi ya Township Rollers mchezo uliopigwa uwanja wa Taifa ukiisha kwa sare ya bao 1-1
Hata hivyo Yanga ilifanikiwa kushinda kwa bao 1-0 kwenye mchezo uliopigwa nchini Botswana
Bado Yanga imeendelea na mwenendo wake wa kutofanya vizuri kwenye michezo ya nyumbani lakini kupata matokeo inapocheza ugenini
Zahera amzungumzia kamusoko
Kiungo wa zamani wa Yanga Thabani Kamusoko ndiye aliyefunga bao la kusawazisha la ZESCO kwenye dakika za majeruhi
Zahera amesema alitumia vyema nafasi aliyopata, hata hivyo hakuipa usumbufu wowote timu yake
"Kamusoko ni mchezaji wa kawaida sana, hakutusumbua kabisa ila yule namba 25 na Winston Kalengo walikuwa mwiba kwetu," amesema

No comments:
Post a Comment