VIDEO: MAGOLI YOTE YANGA SC 1-1 ZESCO UNITED (CAF CL - 14/9/2019)
Yanga SC ‘timu ya wananchi’ wamelazimishwa sare ya bao 1-1 na Zesco United ya Zambia katika mchezo wa Ligi ya mabingwa Afrika uliopigwa leo kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Yanga wamepata bao lao kwa mkwaju wa penati dakika ya 25 kupitia kwa Patrick Sibomana baada ya mshambuliaji wake Sadney kuangushwa kwenye eneo la hatari lakini kiungo wa zamani wa timu hiyo Thaban Kamusoko akaisawazishia Zesco sekunde chache kabla ya mchezo kumalizika ikiwa ni dakika ya 90+4.
Timu hizo zitarudiana wiki mbili zijazo nchini Zambia ambapo Yanga italazimika kushinda au kupata sare ya kuanzia mabao 2-2 ili kuingia hatua ya makundi ya michuano hiyo.
Bonyeza play hapa chini kutazama zaidi pia tembelea app hii kila Mara kusoma habari mpya
No comments:
Post a Comment