We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Wednesday, August 28, 2019

Zahera awapa neno kali wachezaji wapya

Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga, Mwinyi Zahera amewapa tahadhari wachezaji wake wapya waliosajiliwa msimu huu kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania bara VPL.

Yanga iko nyumbani katika Uwanja wa Taifa leo kucheza na Ruvu Shooting, kwenye mchezo wa kwanza wa ligi.
Kuelekea mchezo huo, kocha Zahera amesema amewaambia wachezaji wake wapya kutodharau mechi yoyote, huku akisisitiza kuwa wachezaji wa Kimataifa ambao hawakucheza mechi za Klabu Bingwa Afrika kwa sababu ya vibali, wako fiti kucheza mechi za ligi.
"Nimewaambia wachezaji wote wapya kwamba hakuna hata siku moja Yanga inacheza mechi nyepesi, mechi zote ni ngumu", amesema kocha Zahera.
"Wachezaji wote ambao hawakupata leseni za kucheza mechi za CAF wote watakuwa na nafasi ya kucheza ligi. Wachezaji wote wako vizuri", ameongeza.
Yanga imerejea usiku wa kuamkia Jumatatu kutoka nchini Botswana ambako ilicheza mechi ya marudiano na Township Rollers na kufanikiwa kuvuka hatua ya pili ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika kwa utofauti wa bao moja.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list