We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Friday, August 30, 2019

Zahera ampa Molinga mechi tano


KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema atampa mechi tano mfululizo straika wake, David Molinga ‘Ndama’ ili kiwango chake kiendelee kuwa imara.

Molinga alicheza mechi ya kwanza juzi Jumatano tangu asajiliwe na timu hiyo ambapo alimpa dakika zote 90 za mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ruvu Shooting ambapo walifungwa bao 1-0.
Zahera alisema atampa mechi hizo mfululizo kwani anaamini ni mchezaji mzuri ambaye atafanya vyema kwenye timu yake.
“Siku mbili kabla ya kukamilisha usajili wa Ligi Kuu, nilipata taarifa kuwa Molinga anamaliza mkataba na timu yake ya zamani kwa vile nilikuwa namfahamu niliamini anaweza kuwa bora na kuisadia Yanga msimu huu,”
“Wakati tunakamilisha utaratibu wa usajili wake tena siku ya mwisho Molinga hakuwa anafanya mazoezi kwani alikuwa mapumziko baada ya kumaliza kucheza ligi na ameongezeka uzito, tulimsajili na anaendelea kufanya mazoezi ya mwili huku ligi ikiwa inaendelea.
“Tangu amekuja nchini mpaka sasa amepunguza kilo tano, naamini nikimpa mechi nyingine tano mfululizo za kimashindano na ratiba yake ya mazoezi ngumu anayoifanya atakuwa bora na hata hao wanaombeza wataacha.
Molinga alisema “Si muda wa kuangalia mashabiki wanasema nini kwani sijafuata hayo.”“Namfahamu Molinga, kabla ya kumleta hapa nchini naelewa katika uwezo wake na kama akianza kufanya kile ambacho nakifahamu akiwa DR Congo sioni sababu ya kushindwa kufunga mabao mengi kama ambavyo alikuwa akifanya Heritier Makambo msimu uliopita,” alisema Zahera.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list