We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Sunday, August 4, 2019

Zahera 'afunguka' sare dhidi ya Sharks

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema mchezo dhidi ya Kariobangi Sharks ulikuwa kipimo sahihi kwa wachezaji wake baada ya mazoezi mkoani Morogoro
Yanga leo imelazimishwa sare ya bao 1-1 na Sharks katika mchezo wa kuhitimisha wiki ya Mwananchi uliopigwa uwanja wa Taifa
Zahera amesema changamoto kubwa aliyoiona leo ni tofauti ya utimamu wa mwili wa wachezaji kutokana na kuanza mazoezi kwa nyakati tofauti
"Wachezaji wetu walianza mazoezi siku tofauti mfano Sadney lakini leo amefanya vitu vizuri angewahi mapema angefanya vitu vizuri zaidi," amesema
"Mechi hii ni ya kwanza kubwa kwa wachezaji wangu, kabla tulicheza mechi ndogo ndogo"
"Tunahitaji michezo mingine kujiweka sawa kabla ya tarehe 10"
Aidha Zahera amefurahishwa na mashabiki walioujaza uwanja wa Taifa na kuwataka waendelee na mwenendo huo kwani msimu huu utakuwa wa furaha kwao
"Mwaka huu ni tofauti na mwaka jana, mashabiki waendelee kuja kwa wingi kwani hata kikosi changu cha mwaka huu hakuna anayetembea, nna kikosi kizuri sana"
Kariobangi Sharks ni moja ya timu bora katika ukanda wa Afrika Mashariki kwa sasa
Ni mwezi uliopita tu mabingwa hao wa Sportpesa Cup waliifunga Everton inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza kwa mikwaju ya penati baada ya kutoka nayo sare ya bao 1-1
Mchezo wa leo utamsaidia Zahera kufahamu mapungufu ya kikosi chake na kufanya maboresho kabla ya kuikabili Rollers wiki ijayo

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list