Uongozi wa klabu ya Yanga umeomba mchezo wake wa kwanza wa ligi kuu ya Tanzania Bara ambao umepangwa kupigwa August 28, usogezwe mpaka August 30 kutokana mabingwa hao wa kihistoria kukabiliwa na ratiba ya mchuano ya ligi ya mabingwa
Yanga iko nchini Botswana ambapo Jumamosi ijayo August 24 2019 itashuka dimbani kuikabili Township Rollers
Kulingana na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano Saad Kimji, Yanga inatarajiwa kuondoka Botswana usiku wa kuamkia August 27
Hivyo kutokana na ufinyu wa muda, haitakuwa rahisi wao kurejea August 27 kisha August 28 washuke tena dimbani
Yanga itafungua ligi kwa kuumana na Ruvu Shooting katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Taifa/Uhuru

No comments:
Post a Comment