We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Tuesday, August 20, 2019

Madereva Wa Daladala Kituo Cha Sabasaba Dodoma Waleta Mgomo Kisa Machinga Kuzagaa Kituoni Hapo.

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Madereva  Wa  Daladala katika kituo cha daladala  sabasaba  jijini Dodoma  wamegoma kufanya safari wakishinikiza wamachinga kuondolewa kutokana na ufinyo wa nafasi katika eneo hilo.
Wakizungumza na waandishi wa habari hapo jana Agosti 19,2019  baadhi ya madereva wamesema kuwa,wamegoma kutokana na machinga kutokuwa na utaratibu mzuri wa kufanya biashara.
Baadhi ya abiria waliokuwa wakifanaya safari zao za kutoka na kuingia ndani ya stand hiyo wanaeleza athari za mgomo huo,kama anavyoeleza Franco Jameswakiwa na wenzake.
Akizungumza na madereva hao mkurugenzi wa jiji la Dodoma Godwin Kunambi mbali na kuomba madereva hao kuendelea kusafirisha, amepiga marufuku baadhi ya biashara ikiwemo uchomaji mshikaki .
Mgomo huo Ulimalizika na shughuli zikaendelea kama kawaida katika kituo cha daladala cha SABASABA jijini  Dodoma baada ya Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Godwin Kunambi kuingilia kati na kuamru wafanyabiashara hususan wakaanga mishikaki kutofanyia biashara katika kituo hicho.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list