Kikosi cha Yanga kimemaliza kambi ya siku tatu mkoani Kilimanjaro na kinaelekea mkoani Arusha kufanya maandalizi ya mwisho kabla ya mchezo wa marudiano ligi ya mabingwa dhidi ya Townshipa Rollers
Yanga ilimaliza kambi Moshi kwa kukubali kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Polisi Tanzania
Kesho Yanga itashuka uwanja wa Sheikh Amri Abeid kucheza mchezo wa Kimataifa wa kirafiki dhidi ya AFC Leoprads
Mchezo huo utakuwa wa mwisho kabla ya safari ya kuelekea Botswana siku ya Jumanne
Kocha wa mabingwa hao wa kihistoria Mwinyi Zahera amesema kesho atatumia kikosi tofauti na kile kilichopoteza mchezo dhidi ya Polisi Tanzania jana
Pengine kikosi hicho ndicho kitakachoikabili Township Rollers Jumammosi ijayo huko Botswana

No comments:
Post a Comment