Uzinduzi wa msimu mpya wa ligi kuu ya Tanzania Bara unafanyika leo kwa mchezo wa kukata na shoka kupigwa kati ya mabingwa wa msimu uliopita Simba Sc dhidi ya Azam Fc, mabingwa wa kombe la FA (ASFC)
Ni mchezo unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka nchini, utapigwa saa moja usiku
Wekundu wa Msimbazi ndio wanaoshikilia ngao hiyo waliyoitwaa msimu uliopita baada ya kuifunga Mtibwa Sugar mabao 2-1 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza
Simba imetwaa Ngao hiyo kwa misimu miwili mfululizo
Msimu uliopita ulikuwa bora zaidi kwa Simba dhidi ya wapinzani wao Azam Fc ambapo katika michezo miwili waliyokutana kwenye ligi, Simba ilishinda mmoja na kutoka sare mwingine
Kocha Patrick Aussems hajapoteza mchezo dhidi ya Etienne Ndayiragije
Msimu uliopita Ndayiragije alikuwa na KMC, ambapo mechi zote dhidi ya Simba ziliisha kwa ushindi wa mabao 2-1 kwa Aussems
Licha ya kuutumia mchezo huo kama maandalizi ya mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya UD Songo, inayotarajiwa kuchezwa Agosti 25, Aussems amesema wanahitaji kuanza msimu vizuri kwa kutwaa Ngao ya Jamii
Aidha mashabiki wengi wa Simba wataiongezea timu yao mzuka wa kupata ushindi kwenye mchezo huo
Juzi msemaji wa Azam Fc Jafari Idd Maganga alikiri kuwa hautokuwa mchezo mwepesi kwao kutokana na ukubwa wa Simba SC, anajua changamoto kubwa itakuwa ni idadi ya mashabiki wa Simba SC ndani ya uwanja huo

No comments:
Post a Comment