We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Saturday, August 17, 2019

Waziri Ummy awatoa hofu ndugu wa majeruhi wa ajali ya moto


Wazira wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, amewatembelea majeruhi wa ajali ya moto iliyotokea mkoani Morogoro wanaoendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).

Wakati huo huo ameipongeza Hospitali ya Taifa ya Muhimbili(MNH) kwa huduma nzuri inayotoa kwa majeruhi hao, kwa kuwa wengi waliohamishiwa hospitalini hapo kutoka Morogoro ni wale ambao waliungua kwa kiasi kikubwa sana.

Pia amewatoa wasiwasi ndugu na jamaa wa majeruhi ambao wanaendelea kupatiwa matibabu hospitalini hapo kuwa aina ya matibabu wanayopatiwa ni ya kiwango cha juu.

Pia ameielekeza Hospitali ya Taifa Muhimbili kubadili kitengo cha matibabu ya ajali za moto kuwa kituo maalumu cha kushughulikia ajali za moto.

Akielezea maendeleo ya hali za majeruhi hao, Mkuu wa idara ya magonjwa ya dharura hospitalini hapo Dkt. Juma mfinanga amesema kuwa kwa sasa hivi idadi ya majeruhi ni 21 kati ya 46 waliopokelewa na wote wamehamishiwa katika wodi inayohitaji uangalizi maalum (ICU) kwa ajili ya ufuatiliaji wa karibu wa afya zao.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list