We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Saturday, August 17, 2019

Bashe ataka Bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko kuwa kiungo cha biashara ya mazao Baina ya Kenya na Tanzania

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
NAIBU Waziri wa Kilimo, Mhe. HusseinBashe amesema kikao cha kwanza baina ya timu ya wataalamu wa masuala ya Mazao ya Chakula hapa nchini ikiongozwa na Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB) na ya wenzao kutoka Kenya zinakutana hapa nchini leo Agosti 17, 2019 ili kujadiliana namna bora ya kufanya biashara ya mazao hayo.

Akizungumza na waandishi wa habarijana usiku Agosti 16, 2019 kwenye ofisi za Kituo cha Uwekezaji Nchini (TIC), jijini Dar es Salaam, Mhe. Bashe alisema, kikao hicho ni makubaliano baina ya nchi hizo mbili kukutana na kujadili namna gani wafanyabiashara wa Kitanzania na wenzao wa Kenya watafanya  biashara ya mazao ya chakula na iwe biashara endelevu.

“Biashara tayari imekwisha anza na wakati tunaendelea mpaka sasa wenzetu wa Kenya wamekwishanunua jumla ya tani 34,000 kupitia kwa wafanyabiashara wetu na biashara hiyo inaendelea.” Alifafanua.

Alisema timu ya wataalamu kutoka Tanzania itaongozwa na watu kutoka Wizara ya Kilimo, Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Mamlaka ya Viwango Tanzania (TBS) ili wakae chini na wakubaliane utaratibu wa namna gani  wafanyabiashara wa Tanzania na wenzao wa Kenya watafanya biashara ya mazao ya chakula.

“Sisi Wizara ya Kilimo jukumu letu ni kufanya mambo makubwa mawili, kuhamasisha uzalishaji wa mazao na kufungua masoko ya wakulima wetu ili waweze kufanya biashara.” Alifafanua.

Alisema katika kikao hicho wametaka mamlaka za viwango za Kenya na Tanzania zijumuishwe kwenye majadiliano hayo ili wazalishaji wa sembe waliosajiliwa Tanzania waweze kusajiliwaKenya Bureau of Standards ili bidhaa zao ziweze kwenda katika soko la Kenya bilavikwazo vyovyote.

“Tunatengeneza Government Agreement ambayo itaonyesha mpango kazi (frame work) ya namna biashara hii itafanyika, tumeshaiteua Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko ambayo ndiyo itakayokuwa kiongozi msimamizi na kiungo wezeshi katika biashara hiyo.” Alibainisha Mhe. Bashe.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list