We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Wednesday, August 28, 2019

Waziri Jafo Atangaza Majina ya Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga Na Kidato Cha Tano Awamu Ya Pili 2019

Serikali imewachagua wanafunzi 1,674 kujiunga kidato cha tano baada ya awamu ya kwanza kukosa fursa hiyo.

Katia  uchaguzi wa Awamu ya kwanza,serikali ilitangaza kuwa wasichana wote waliofaulu kidato cha nne walichaguliwa kujiunga vyuo mbalimbali pamoja na kidato cha sita lakini wavulana 1,861 hawakuchaguliwa licha ya kuwa na sifa.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo ametangaza hayo leo, Jumatano (Agosti 28, 2019), jijini Dodoma huku akisema kuwa 187 wamekosa kwa kukosa uwiano katika tahasusi zao.

Waziri  Jafo amesema wanafunzi hao wanatakiwa kuanza kuripoti katika shule walizochaguliwa kuanzia Septemba 2 hadi 16,2019 huku akiwataka waliokosa nafasi kutokata tamaa badala yake waombe vyuo vya kati ili wajiunge.

Ametaja sababu za kupatikana kwa nafasi ni kutokana na baadhi ya wanafunzi kujiunga shule binafsi na baadhi ya shule zimeongeza majengo.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list