Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema kupoteza mchezo wa kwanza wa ligi kuu leo dhidi ya Ruvu Shooting kumetokana kwa kiasi kikubwa na uchovu wa wachezaji wake
Akizungumza baada ya mchezo huo uliomalizika kwa Yanga kufungwa bao 1-0, Zahera ameitupia lawama Bodi ya ligi kwa kuipangia timu yake ratiba isiyo rafiki
Awali uongozi wa Yanga uliomba mchezo huo usogezwe mbele lakini Bodi ya ligi ilikataa maombi hayo
"Sisi tumecheza Botswana tarehe 24, tumetumia siku mbili kufika hapa Tanzania. Wachezaji wangu hawakupata mapumziko ya kutosha, tumefanya mazoezi siku moja leo tumeingia uwanjani" amesema
"Inashangaza kuona sisi tuliotoka mbali tumepaswa kucheza mapema kabla ya Simba ambayo ilicheza hapahapa Tanzania"
"Matokeo haya hainishangazi, mmeona Sibomana, Balinya, Urikhob, Lamine wote walikuwa wamechoka"

No comments:
Post a Comment