We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Monday, August 19, 2019

Uamuzi malipo ya waliopisha ujenzi Terminal III

Hatimaye wananchi  wa Kipunguni waliopisha upanuzi wa Jengo la tatu la Abiria katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere,  wameanza kugawiwa maeneo yao hii ni baada ya kuwepo kwa mgogoro wa makubaliano kati ya kampuni ya kupima viwanja ya Tanzania Remix na wamiliki halali.

Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Atashasta Nditiye, wakati akizungumza na EATV & Radio Digital na kusema kuwa, hadi sasa takribani viwanja zaidi ya 400 vilivyopo kata ya Msongola  vimekwishagawiwa.
''Sisi Tanzania Remix walitupatia baadhi ya viwanja na  bado tunawadai vichache sana na wako kwenye taratibu za mwisho za kuhakikisha,  hivyo vichache vilivyobakia kati ya 537 vinakamilika ili wananchi wale waliopisha upanuzi wa kiwanja cha ndege waweze kupatiwa viwanja vyao'',  amesema Naibu Waziri.
Serikali kupitia Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini (TAA), imekwishailipa Kampuni ya Tanzania Remix kiasi cha shilingi bilioni 3.7 kwa ajili ya viwanja 537,  vitakavyolipwa fidia kwa wananchi wa Kipunguni na Kigilagila waliopisha mradi huo.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list