Kiungo mpya wa Simba Francis Kahata amesema wana matumaini makubwa ya kufanya vizuri kwenye ligi na michuano mbalimbali watakayoshiriki kutokana na maandalizi waliyofanya
Kahata aliyetua Simba akitokea klabu ya Gor Mahia ya Kenya, amesema kambi waliyoweka Afrika Kusini ilikuwa na mafanikio
"Kambi yetu ilikuwa nzuri Afrika Kusini. Tumefanya maandalizi mazuri, wachezaji tuko tayari kuwapa burudani mashabiki wetu," amesema
"Mashabiki waendelee kutuunga mkono, tutaipigania timu kuhakikisha tunapata matokeo mazuri kwenye kila mchezo"
Kahata atatambulishwa rasmi Msimbazi August 06 siku ya Tamasha la Simba Day ambapo siku hiyo Simba itacheza na Power Dynamos ya Zambia
Wachezaji wengine ambao itakuwa mara yao ya kwanza kushiriki Tamasha hilo ambalo limekuwa likifanyika kwa miaka 10 sasa ni pamoja na Beno Kakolanya, Wilker Da Silva, Gerson Fraga, Tairone Santos, Sharaf Shiboub, Kennedy Juma, Gadiel Michael na Deo Kanda
Ibrahim Ajib, Miraji Athumani na Haruna Shamte waliwahi kushiriki Tamasha hilo wakiwa wachezaji wa Simba kabla ya kuondoka na sasa wamerejea tena

No comments:
Post a Comment