We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Tuesday, August 6, 2019

TETESI ZA USAJILI BARANI ULAYA LEO JUMANNE

Everton wamekusanya 'kapu' la usajili lenye thamani ya pauni milioni 100 kumsajili msahambuliaji wa Crystal Palace Wilfried Zaha, 26. Ofa hiyo inahusisha pia Everton kuwapa Palace mshambuliajii Cenk Tosun na kiungo James McCarthy, wote wana miaka 28. (Sun)
Zaha ambaye ni raia wa Ivory Coast anatarajiwa kujiunga na Everton kabla ya Alhamisi ambapo diisha la usajili Uingereza linafungwa, Palace wapo tayari kupokea kitita cha kufikia pauni milioni 65. (Independent)
Arsenal wanaweza kuelekeza nguvu zao zote katika kumsajili beki wa kati wa RB Leipzig Mfaransa Dayot Upamecano, 20, kama mbadala wa beki wa Juventus Daniele Rugani - lakini Leipzig wanataka pauni milioni 50 ili kumuachia beki huyo. (Mirror)

Paul Pogba
Image captionPaul Pogba

Juventus wanajiandaa kuwapa Manchester United wachezaji watatu ili kubadilishana na kiungo Paul Pogba. (Mirror)
Mpango huo kama utafaulu, utawahusisha wachezaji Danilo, 28, na Joao Cancelo, 25. (Goal.com)

Nathan Ake
Image captionJe, Ake anastahili kuuzwa kwa pauni milioni 75?

Leicester haitamsajili Nathan Ake katika dirisha hili la usajili baada ya klabu ya Bournemouthkutaka dau la pauni milioni 75 kwa beki huyo raia wa Uholanzai. (Sky Sports)
Arsenal wamejaribu kufikia makubaliano na nahodha wao Laurent Koscielny - lakini beki huyo mwenye miaka 33, ambaye aligoma kusafiri na timu kwenda Marekani, pia amegoma kufanya mazungumzo na klabu. (Mirror)

Romelo Lukaku
Image captionRomelo Lukaku

Manchester United wataendelea kupokea ofa kwa ajili ya mshambuliaji wao Romelu Lukaku, 26, lakini yawezekana wasitafute mbada wake endapo ataondoka baada ya kuchipukia kwa kinda Mason Greenwood, 17. (ESPN)
Lukaku ana uwezekano mkubwa wa kujiunga Inter Milan kuliko Juventus hususani endapo Man United itashindwa kumpata Paulo Dybala, 25. (Express)

Christian Eriksen
Image captionEriksen (kulia) amekuwa mwenye kiu ya kuihama Spurs katika dirisha hili la usajili.

Manchester United wanakaribia kumsajili kiungo wa Tottenham raia wa Denmark Christian Eriksen, 27, baada ya kiungo wa Sporting LisbonMreno Bruno Fernandes - ambaye alikuwa anawindwa na Man United kuweka wazi nia yake ya kujiunga na Spurs. (AS)
Tottenham inajiandaa kupokea ofa za kiuhalisia kutoka klabu za Ulaya kwa ajili ya Eriksen endapo mchezaji huyo hatauzwa ndani ya Uingereza mpaka dirisha litakapofungwa nchni humo kesho Alhamisi. (Telegraph)

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list