Tottenham hawana uhakika na nia ya Christian Eriksen kutokana na kuvunjika kwa mahusiano kati ya mwenyekiti wao Daniel Levy na wakala wa kiungo huyo mwenye miaka 27 raia wa Denmark. (Guardian)
Meneja wa zamani wa Tottenham Harry Redknapp anaamini Eriksen anatakiwa kuanza kwenye mechi za Spurs licha ya kutokujulikana kwa hatma yake ya mbeleni. (Talksport)
Mshambuliaji wa Inter Milan Romelu Lukaku, 26 anataka kuondoka Manchester United kwa sababu alichoshwa na klabu hiyo , kwa mujibu wa kocha wa Belgium Roberto Martinez. (Mirror).
Kaka yake Paul Pogba, Mathias mwenye umri wa miaka 29 ambaye ni mshambuliaji wa klabu ya Deportivo Manchego, amesema mdogo wake anayechezea Manchester United itapendeza zaidi kama atahamia Real Madrid. (AS)
PA MEDIA
Mshambuliaji wa Everton Cenk Tosun anataka kubaki katika klabu hiyo licha ya kuwepo kwa tetesi kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 ana mpango wa kuhamia Eintracht Frankfurt. (Turkish Football)
Liverpool imesema kuwa haina mpango wa kumuuza mshambuliaji wake Bobby Duncan na imekataa kutumia mbinu za Fiorentina. (Liverpool Echo)
Mchezaji wa Brighton, Jurgen Locadia, 25 anaweza kusajiliwa kwa mkopo na Bundesliga side Hoffenheim. (Argus)
Olympiakos wako katika mazungumzo na klabu ya Leicester katika mpango mpya wa kumsajili mshambuliaji wa Foxes ambaye ni raia wa Algeria Rachid Ghezzal, 27. (Sky Sports)
Manchester City wapo katika mipango ya kumnasa mlinzi wa klabu ya Hearts Aaron Hickey kwa dau la paundi milioni 1.5 ili kumpata mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 17 ifikapo mwezi Januari. (Sun)
Kiungo wa klabu ya West Bromwich Albion, Rekeem Harper mwenye umri wa miaka 19 amepewa nafasi kubwa katika mipango ya kocha mkuu wa klabu hiyo Slaven Bilic katika msimu huu. (Express and Star)

No comments:
Post a Comment